SERIKALI YAANDAA MUSWADA WA TARATIBU ZA UVUNAJI NA UPANDIKIZAJI VIUNGO VYA BINADAMU

Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel amesema kutokana na kuongezea kwa mahitaji ya upandikizaji wa viungo Nchini, Serikali imeandaa Muswada wa kutunga Sheria itakayoongoza taratibu za uvunaji, utunzaji na upandikizaji wa viungo. Ameeleza hayo akimjibu Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve, aliyehoji kuhusu mkakati wa Serikali kuanzisha utaratibu maalum wa kuvuna viungo vya binadamu kama